ActEarlyASDFactSheetSWAHILI.txt

Plain Text icon ActEarlyASDFactSheetSWAHILI.txt — Plain Text, 8 KB (8978 bytes)

File contents

Spektra ya Ugonjwa wa Tawahudi 

KARATASI YA UKWELI 

 

 Autism Spectrum Disorder Fact Sheet (Swahili) 

 

 

 

 

Spektra ya tawahudi (Spektra ya ugonjwa wa akili 
wa watoto) ni nini? 

Spektra ya tawahudi (spektra ya ugonjwa wa akili wa watoto) (ASD) ni 
ulemavu wa ukuaji unaosababishwa na matatizo ya kiakili. 
Wanasayansi bado hawajui hasa kinachosababisha matatozi haya kwa 
watu wengi walio na ASD. Hata hivyo, baadhi ya watu walio na ASD 
wana matatizo yanayojulikana, kama vile hali ya kijenetiki. 

 Kuna sababu nyingi zinazosababisha ASD, ingawa nyingi bado 
hazijulikani. 

 

Huwa hakuna kitu kinachohusu jinsi watu walio na ASD wanakaa kinacho 
watofautisha na watu wengine, lakini wanaweza kuwasiliana, kuingiliana, 
kuwa na tabia tofauti na kujifunza kwa njia zilizotofauti na watu wengine. 
Uwezo wa kujifunza, kufikiria, na utatuzi wa tatizo wa watu walio na ASD 
unaweza kulingana kutoka kwa wenye kipaji hadi walioathirika sana. 

Baadhi ya watu walio na ASD wanahitaji msaada zaidi maishani mwao; 
wengine wanahitaji msaada kidogo. 

 

Ubainishaji wa ASD sasa unajumuisha hali kadhaa zilizokuwa 
zinabainishwa kando: ugonjwa wa akili, ugonjwa wa ukuaji unaoenea 
kote ambao bado haujabainishwa (PDD-NOS), na ugonjwa wa Asperger. 
Hali hizo zote sasa zinajulikana kama spektra ya ugonjwa wa akili. 

 

Baadhi ya dalili za ASD ni zipi? Watu walio na ASD mara kwa 
mara huwa na matatizo ya kijamii, mhemuko, na mawasiliano. Wanaweza 
kurudia tabia fulani na huenda wasitake mabadiliko katika utaratibu wao 
wa kila siku. 

Watu wengi walio na ASD pia wana njia tofauti za kujifunza, kuwa makini, 
au mwitiko wao kwa mambo. Dalili za ASD huanza wakati wa utotoni na 
humuathiri mtu maishani mwake mwote. 

 

 

Watoto au watu wazima walio na ASD huenda: 

. wasilenge kitu kwa kidole ili waonyeshe kuwa wanavutiwa (kwa mfano, 
wasilenge ndege inayopita juu yao) 
. wasiangalie vitu wakati mtu mwingine anavilenga kwa kidole 
. wawe na tatizo la uingilianaji na watu wengine au wasivutiwe kabisa 
na watu wengine 
. waepuke kuangaliana macho kwa macho na watake kuwa peke yao 
. wawe na tatizo la kuelewa hisia za watu wengine au kuzungumza kuhusu 
hisia zao 
. wasitake kushikiliwa au kukumbatiwa, au wanaweza kukumbatiwa 
wanapotaka tu 
. waonekane kama hawajui wakati watu wanazungumza nao, lakini wanajibu 
sauti za vitu vingine 
. wavutiwe na watu sana, lakini wasijue kuzungumza, kucheza, au kuingiliana 
nao 
. warudie maneno au misemo wanayoambiwa, au warudie maneno au 
misemo badala ya lugha ya kawaida 
. wawe na tatizo la kuelezea mahitaji yao kwa kutumia maneno au ishara za 
kawaida 
. wasicheze michezo ya �kuigiza� (kwa mfano, wasiigize kwamba �wanalisha� 
mtoto wa bandia) 
. warudie vitendo mara kwa mara 
. wawe na tatizo la kuzoea utaratibu mpya mambo yanapobadilika 
. kuwa na mwitiko tofauti wa vile vitu vinanuka, kuonja, kuonekana, 
vinavyohisi, au kusikika 
. wakapoteza ujuzi waliokuwa nao (kwa mfano, kuwacha kusema maneno 
waliyokuwa wanatumia) 


 

Ni nini ninachoweza kufanya ikiwa ninadhania 
mtoto wangu ana ASD? 

Zungumza na daktari au muuguzi wa mtoto wako. Ikiwa wewe au daktari 
wako anadhani kunaweza kuwa na tatizo, agiza kwamba mtumwe kwa 
daktari wa ukuaji wa watoto au mtaalamu mwingine. 

Wakati huohuo, wasiliana na uajenti wako wa karibu wa ukaguzi wa 
mapema (kwa watoto walio na umri chini ya miaka 3) au shule ya 
umma ya karibu (kwa watoto walio na umri wa miaka 3 na 
kuendelea), hata kama mtoto wako huwa haendi shule hiyo. 

 Ili ujue utakayezungumza naye katika eneo lako, wasiliana na Kituo cha 
Taarifa cha Kitaifa kwa Watoto na Vijana Walio na Ulemavu (National 
Information Center for Children and Youth with Disabilities) kwa kuingia 
kwenye www.nichcy.org. Zaidi ya hayo, Vituo vya Udhibiti na Uzuiaji 
Ugonjwa (Centers for Disease Control and Prevention) una viungo kwenye 
ukurasa wake wa tovuti ya Spektra ya Ugonjwa wa Kiakili kuhusu taarifa 
kwa familia (http://www.cdc.gov/ncbddd/autism/links.html). 

 

Usisubiri. Kuchukua hatua mapema kunaweza kuwa na manufaa makubwa! 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

www.cdc.gov/actearly | 1-800-CDC-INFO 

 

 

 

 

 

Elewa Dalili. Chukua Hatua Mapema 


Hoja informativa sobre el trastorno del 
espectro autista (TEA) 

 

 

 

 

 

�Qu� son los trastornos del espectro autista? Los 
trastornos del espectro autista (TEA) son discapacidades del 
desarrollo causadas por diferencias en el cerebro. Los cientIficos a6n 
no saben con exactitud qu� causa estas diferencias en la mayorIa de 
las personas con TEA. Sin embargo, algunas personas con estos 
trastornos tienen una diferencia conocida, como una afecci�n 
gen�tica. Los TEA tienen m6ltiples causas, pero la mayorIa a6n se 
desconoce. 

 

Por lo general, no se puede notar ninguna diferencia en el aspecto de 
una persona con TEA, pero es probable que tenga maneras de 
comunicarse, interactuar, comportarse y aprender distintas a las de 
la mayorIa de las personas. Las aptitudes mentales y la capacidad de 
aprendizale de quienes tienen TEA, asI como su capacidad para 
resolver problemas, pueden variar; hay desde personas talentosas 
hasta otras con problemas muy serios. Algunas personas con TEA 
necesitan mucha ayuda en su vida cotidiana; otras requieren menos. 

 

En la actualidad, el diagn�stico de los TEA incluye varias 
afecciones que antes solIan diagnosticarse por separado: el 
trastorno autIstico, el trastorno generalizado del desarrollo 

no especificado de otra manera (PDD-NOS, por sus siglas en ingl�s) 
y el sIndrome de Asperger. Todas estas afecciones se llaman ahora 
trastornos del espectro autista. 

 

�Cu�les son algunos de los signos de los TEA? Las 
personas con TEA a menudo tienen problemas sociales, emocionales 
y de comunicaci�n. Tambi�n es probable que repitan ciertas 
conductas y que no quieran cambiar sus actividades diarias. Muchas 
personas con TEA tambi�n tienen diferentes maneras de aprender, 
prestar atenci�n o reaccionar ante las cosas. Los signos de los TEA 
comienzan en la primera infancia y perduran toda la vida de una 
persona. 

 

Puede que los ni�os o adultos con TEA: 

� No se�alen obletos para mostrar inter�s (por elemplo, 
puede que no se�alen un avi�n que pase volando). 

� No miren los obletos que otra persona se�ala. 

� Tengan problemas para relacionarse con otros o no est�n 
interesados en otras personas para nada. 

� Eviten mirar a los olos y prefieran estar solos. 

 

 

� Tengan problemas para comprender los sentimientos de 
otras personas o para expresar sus propios sentimientos. 

� Prefieran que no los abracen o permitan que lo hagan solo 
cuando ellos lo desean. 

� Aparenten no percatarse cuando las personas les hablan, pero 
respondan a otros sonidos. 

� Est�n muy interesados en otras personas, pero no sepan 
c�mo hablarles, lugar o establecer contacto con ellas. 

� Repitan palabras o frases que se les digan, o repitan palabras o 
frases en vez de usar la forma normal del lenguale. 

� Tengan problemas para expresar sus necesidades mediante 
palabras o movimientos tIpicos. 

� No lueguen a imitar a los grandes (por elemplo, puede que no 
lueguen a darle de �comer� a una mu�eca). 

� Repitan las mismas acciones una y otra vez. 

� Tengan problemas para adaptarse a cambios en la rutina. 

� Reaccionen de forma extra�a a la manera en que las cosas 
huelen, saben, se ven, se sienten o suenan. 

� Pierdan las destrezas que en alg6n momento tuvieron 
(por elemplo, puede que delen de decir palabras que 
estaban usando anteriormente). 

 

�Qu� puedo hacer si creo que mi hijo tiene 
TEA? 

Hable con el m�dico o enfermero de su hilo. Si usted o su doctor 
piensan que podrIa haber un problema, pida que remitan a su hilo 
a un pediatra especializado en desarrollo infantil o a otro 
especialista. Al mismo tiempo, comunIquese con su agencia local 
de intervenci�n temprana (para ni�os menores de 3 a�os) o con 
su escuela p6blica (para ni�os 

de 3 a�os o m�s), aun cuando su hilo no vaya a ese 
establecimiento. Para averiguar con qui�n debe hablar en su �rea, 
visite el sitio web del Centro Nacional de Diseminaci�n de 
Informaci�n para Ni�os con Discapacidades (NICHCY, por 

sus siglas en ingl�s) en http://nichcy.org/espanol. Adem�s, 

los Centros para el Control y la Prevenci�n de Enfermedades 
(CDC) tambi�n tienen informaci�n para las familias en su p�gina 
web sobre los trastornos del espectro autista 

(http://www.cdc.gov/ncbddd/Spanish/autism/links.html). 

 

INo espere! IReaccionar pronto puede hacer una gran diferencia! 

 

 

 

 

 

www.cdc.gov/pronto | 1-800-CDC-INFO 

 

 

 

 

 

 

Aprenda los signos. Reaccione pronto.